Kuganda kwa asali ni tabia ya asali kubadilika na
kutengeneza chengachenga. Tabia hii inatokana na viundo vya asali na namna
ilivyohifadhiwa. Aina nyingine ya asali haigandi wakati nyingine huganda mara
tu baada ya kukamuliwa au hata ikiwa bado kwenye masega. Aina kuu mbili za
sukari zilizomo kwenye asali (fruktosi na glukosi) ndizo zinazosababisha
kuganda kwa asali. Kadiri kiwango cha glukosi kinavyoongezeka ndivyo asali
inavyoganda kwa haraka na kiwango kikubwa cha fruktosi huchelewesha kuganda kwa
asali. Vitu vingine vinavyosababisha kuganda kwa asali ni kushuka kwa joto,
asali kuwa na ukungu na aina ya mimea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni