Alhamisi, 16 Julai 2015

Kuganda kwa Asali


        
Kuganda kwa asali ni tabia ya asali kubadilika na kutengeneza chengachenga. Tabia hii inatokana na viundo vya asali na namna ilivyohifadhiwa. Aina nyingine ya asali haigandi wakati nyingine huganda mara tu baada ya kukamuliwa au hata ikiwa bado kwenye masega. Aina kuu mbili za sukari zilizomo kwenye asali (fruktosi na glukosi) ndizo zinazosababisha kuganda kwa asali. Kadiri kiwango cha glukosi kinavyoongezeka ndivyo asali inavyoganda kwa haraka na kiwango kikubwa cha fruktosi huchelewesha kuganda kwa asali. Vitu vingine vinavyosababisha kuganda kwa asali ni kushuka kwa joto, asali kuwa na ukungu na aina ya mimea.

Jumatano, 8 Julai 2015

ASALI inafahamika kwa muda mrefu kama chakula muhimu ambacho pia kinasaidia sana katika kupambana na magonjwa mbalimbali na matatizo yatokanayo na uzee. Kwa mujibu wa tafiti mpya za wataalamu wa madawa lishe na vifaa tiba, imedhihirika kwamba, uwezo wa asali kutibu unaweza kuongezeka maradufu kama itachanganywa na mdalasini.

Aidha, uchunguzi wa kila wiki unaofanywa na jarida la World News kuhusu tiba unasema, wataalamu wa madawa yatokanayo na mimea,imeonekana kwamba kuna dazani nyingi za umuhimu wa asali na mdalasini katika kujenga afya bora.

Asali ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta ya vuguvugu ya mzaituni, hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele kinachotumika katika dawa ya Dork.

Mchanganyiko huo vuguvugu unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15. Kwa mujibu wa watafiti wa madawa tiba, Dk Alexander Andreyed na Eric Vogelmann, madhara yaletwayo na vyakula vyenye mafuta mwilini yanaweza kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa kwa matumizi ya mara kwa mara ya chai iliyoungwa kwa kutumia mchanganyiko wa asali na mdalasini.

Ugunduzi wao huo, uliyakinishwa vema kwenye jarida mashuhuri linalozungumzia masuala ya tiba la nchini Denmark la Julai 1994. Uchunguzi mwingine pia umeonesha kwamba matumizi ya kila siku ya asali yanapunguza viwango vya lehemu mwilini.

Asali inatajwa pia kuwa dawa ya jino, inaponya pia ngozi iliyoharibika, ni dawa asilia ya shinikizo la juu la damu ni kiungo muhimu katika utengenezaji wa asilimia kubwa ya madawa mmimiko na asilimia kubwa ya vipodozi na mafuta ya kupaka.

Ugonjwa wa mafua ambao huwakera na kuwanyima watu wengi raha imegundulika na wataalamu kwamba hupungua na kupotea kabisa ikiwa watatumia kijiko kimoja cha chai cha asali vuguvugu iliyochanganywa na robo kijiko cha chai cha mdalasini. Mtafiti mmoja wa Hispania imethibitisha kwamba, aina ya dawa moja asilia iliyofanikiwa kuharibu vimelea viletavyo mafua ilitengenezwa kwa kiwango kikubwa na asali.

Mchanganyiko huo pia ni mahususi katika kusaidia kupunguza na kuondoa chafya na kuvimba kwa koo. Asali inaaminika pia huamsha hamu ya tendo la ndoa. Wale ambao mambo katika eneo hilo si mazuri wanashauriwa angalau kunywa vijiko viwili vya mezani kila siku kabla ya muda wa kulala usiku. Kuna wakati asali ilipigwa marufuku kwa makasisi katika baadhi ya dini za Mashariki mwa dunia ili isiwe sababu ya kuwaongezea mihemko.

Asali inaaminika kuwa dawa ifaayo katika kuondoa mchafuko wa tumbo pamoja na kichefuchefu. Ukiwa katika kadhia hiyo, unashauriwa kuongeza kiasi kidogo cha mdalasini na asali kwenye chai ama maji, itapunguza hali hiyo na maumivu yaletwayo na vidonda vya tumbo.

Utamaduni wa kula asali pamoja na mdalasini, huweza kuondoa mchafuko wa tumbo na utumbo uletwao na gesi kwa mujibu wa uchunguzi mahsusi uliofanywa huko India na Japani kwa miaka mingi. Unaweza kukinga kupata ugonjwa wa moyo na kuzuia, mkusanyiko wa mtandao wa mafuta kwenye mishipa ya damu kwa kula asali na mdalasini mara kwa mara wakati wa kifungua kinywa.

Kula mkate uliopakwa asali kijiko kimoja cha mezani kila siku nyuzi nyuzi zake ni muhimu pia kiafya. Tiba hii, iliweza kupunguza kuganda kwa mishipa ya damu kwa asilimia 74 ya wagonjwa waliofanyiwa utafiti. Shinikizo la damu, pamoja na matatizo yaambatanayo na maumivu ya kifua na kizunguzungu yalitoweka kutoka kwa wagonjwa wengi wiki chache tu baada ya watafiti wa Kiitaliano kuwapa dozi za mara kwa mara za asali iliyochanganywa na mdalasini.

Kinga ya mwili, itaongezeka mara tatu zaidi ikiwa utatumia mara kwa mara asali na mdalasini kwa pamoja, wataalamu wanasema. Utafiti wa kitiba unaonesha kwamba, asali ina hazina kubwa ya virutubisho na madini pamoja na michanganyiko mingine iondoayo magonjwa pamoja na kinga, itolewayo na chembechembe nyeupe za damu, husaidia kuzuia magonjwa pamoja na kuharibu vimelea virusi na bakteria. Vijiko viwili vya asali iliyonyunyiziwa mdalasini kabla ya mlo, huondoa kiungulia pia. Inasemekana kuwa, unaweza kuishi hadi miaka 100 ukifurahia maisha ya afya bora na madhubuti kwa kunywa kila siku kikombe baridi cha chai iliyowekwa mdalasini na asali.

Kutengeneza kinywaji hiki kitamu, weka vijiko vinne vikubwa vya mdalasini katika vikombe vitatu vya maji na koroga kwa dakika 10, kunywa robo kikombe kutwa mara tatu au nne, watafiti wanasema.

Asali ni tiba rafiki na asilia kwa watu wenye shida ya chunusi. Ili kutibu tatizo hilo watafiti wanasema changanya vijiko vitatu vya asali pamoja na kijiko kimoja mdalasini na pakaa kwenye chunusi.

Uwezo wa asali wa kuua bakteria utaufanya uso wako kuwa kawaida katika muda wa wiki mbili pekee. Asali, wanasema inairudisha ngozi iliyoharibiwa na wadudu waharibifu kama dondola, washawasha na hata ngozi iliyopata madhara kutokana na kuungua moto. Pakaa asali na mdalasini moja kwa moja kwenye sehemu zilizoathirika na rudia wakati mwasho unapokuathiri. Rudia tena hadi uvimbe unapotoweka.

Utafiti uliofanywa karibuni nchini Australia na Japan, umeonesha kuwa, asali ina uwezo mkubwa katika tiba ya mgonjwa kwa mtu anayetumia madawa ya kutibu saratani. Katika utafiti uliofanywa kwa wagonjwa waliokuwa wanaugua kwa kiwango kikubwa saratani ya mifupa na tumbo, wale waliokuwa wakitumia kila siku dozi za asali na mdalasini, walionesha kupata nafuu maradufu kuliko wale waliokuwa wakitumia madawa ya saratani pekee. “Tuliwapa kijiko cha mdalasini na asali kutwa mara tatu kwa mwezi,” anasema Dk Hiroki Owatta. Upo ushahidi mpya kwamba, sukari asilia zilizopo kwenye asali, zina uwezo wa kuongeza nishati mwilini. Zikitumika ipasavyo, sukari hizi zinaweza kuwasaidia wazee na wengine wanaosumbuliwa na uchovu.

Wataalamu wanapendekeza kuchanganya nusu kijiko cha asali katika nusu bilauri ya maji kisha nyunyizia mdalasini na kunywa masaa mawili baada ya kuamka asubuhi. “Kunywa tena saa 9:00 alasiri wakati nishati (nguvu) inapoanza kushuka,” anashauri Dk Milton Abbozza ambaye kazi zake kuhusu asali na mdalasini kama kichocheo cha nishati mwilini zinatambulika kimataifa.

Asali inao uwezo mkubwa wa kupunguza na kuponya miguu iliyopasuka kwenye kisigino. Chua asali na mdalasini vuguvugu katika miguu au nyayo zilizoathirika baada ya siku ndefu na kazi au baada ya mazoezi marefu. Rudia kila siku asubuhi halafu, osha nyayo zako kwenye maji baridi na vaa viatu.

Baadhi ya watu Marekani ya Kusini, wanasukutua maji ya vuguvugu yaliyowekwa asali na mdalasini kila asubuhi ili kufanya harufu mdomoni kuwa nzuri na safi kiasilia. Katika Asia ya Kusini Mashariki, watu hutumia kijiko cha mdalasini na asali ili kuondoa harufu mbaya mdomoni (halitosis).

Wataalamu wanaamini kwamba, uwezo wa kuua bakteria uliopo kwenye asali ndiyo unaopigana na harufu mbaya itokayo mdomoni. Dozi za kila siku za asali na mdalasini, hufanya hali ya usikivu murua kwa wanafunzi wawapo darasani au viongozi mkutanoni kama ilivyogunduliwa na Wagiriki wa zamani. Hiyo ndiyo asali. Ni chakula na dawa. Lakini inayozungumzwa hapa ni asali mbichi ambayo inapatikana kwa wingi Tanzania, lakini tatizo kubwa ipo pia feki inayouzwa kama mbichi!

Kwa hisani ya AFYA.KWANZA


Jumatatu, 6 Julai 2015

UMUHIMU WA ASALI, FAHAMU ASALI HALISI NA FEKI

Tunafahamu kwamba asali ina umuhimu mkubwa sana katika mwili wa binaadamu, lakini watu wengi wamekuwa wakipigwa kwa kuuziwa asali feki, sasa leo nimeona niwape darasa wanunuzi wa asali ili wasiweze kununua asali feki.

Maana sehemu nyingi, wafanyabiashara wamekuwa wakiuza asali ambayo haina ubora kwa kuchanganya maji na sukari guru.


1. Njia ya kwanza,

chukua njiti ya kibiriti kisha ichovye sehemu yenye baruti kwenye asali unayotaka kuinunua,

kisha iwashe njiti hiyo kwa kutumia kibiriti chako, ikiwaka, ujue hiyo ni asali kweli.


2. Njia ya pili,

Dondosha asali chini katika mchanga, ukiona sehemu ya mchanga iliyolowana ikijikusanya

pamoja ujue hiyo nii asali orginal.


3. Njia ya tatu,

Chukua karatasi jeupe, dondoshea asali njia juu yake, kama ikichelewa kutokea upande wa pili,

ujue hiyo asali safi na inafaaa kwa matumizi ya binaadamu.


N.B Bado kuna njia nyingine ambayo hutumiwa na baadhi ya watu, kama vile kuimwaga katika kiganja

cha mkono wako, ukiona tone la mwisho linabakia kwenye chupa kuja mkononi, hiyo ni asali nzuri.


Pia wengine huangalia kama ikiwa kwenye chupa huwa inatengeneza alama yenye mfano wa korosho.



" Nadhani hutaibiwa tena kwa kuuzia asali feki".

Ijumaa, 3 Julai 2015

FAHAMU MATUMIZI YA ASALI KWA UPONYAJI WA MISHONO YA OPERATION.

ASALI ni dawa nzuri sana katika kutibu mishono ya operation mbali mbali. Wataalamu wanazidi kuhamasisha matumizi ya asali kwenye mishono kila siku.

Asali imekua inatumika kwa miaka mingi kwasababu zifuatazo:-
1. Ina kiwango kikubwa cha sukari ( High Sugar content) inayofanya bakteria washindwe kuzaliana au kuishi.


2. Ina kiwango kidogo cha unyevu ( Low Moisture content) - hii inafanya kidonda kiwe kikavu


3. Ina HYDROGEN PEROXIDE ambayo inazuia bakteria


4. Gluconic acid ambayo inatengeneza mazingira ya Acid kwenye kidonda na hivyo kuzuia ukuaji wa bakteria.


Faida ya kutumia ASALI kwenye mishono ya operation ni pamoja na:-
1. Inapunguza kuvimba kwa kidonda na pia uvimbe wa kidonda
2. Inaongeza spidi ya uponaji wa kidonda.
3. Inasafisha kidonda


MATUMIZI YAKEUnaweza paka hadi mara mbili kwa siku kuharakisha uponaji, lakini hakikisha asali hiyo ni safi.


ANGALIZOUnashauriwa upate ushauri wa kitaalamu kwanza wa daktari wako kabla ya kujiamulia kupaka mwenyewe nyumbani ili kufanya kitu sahihi.

Jumanne, 30 Juni 2015

Matumizi ya asalibora katika matibabu

Sehemu nyingi duniani watu wanatumia asalibora kutibu magonjwa mbalimbali. Licha ya kuwa asali bora huongeza kinga ya mwili, sayansi ya tiba imebaini asali bora ina wingi wa sukari (76g/ml), tindikali (acidity, Ph = 3.6-4.2) na baadhi ya kemikali ambazo zinatokana na viumbe hai (organic compounds) vyote kwa pamoja ni sababu za asalibora kuwa ni dawa.