Sehemu nyingi duniani watu
wanatumia asalibora kutibu magonjwa mbalimbali. Licha ya kuwa asali bora huongeza
kinga ya mwili, sayansi ya tiba imebaini asali bora ina wingi wa sukari
(76g/ml), tindikali (acidity, Ph = 3.6-4.2) na baadhi ya kemikali
ambazo zinatokana na viumbe hai (organic compounds) vyote kwa pamoja ni
sababu za asalibora kuwa ni dawa.